Psalms 11
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako. 2Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo. 3Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?” 4Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu. 5Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia. 6Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao. 7Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.