Psalms 120
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Wimbo wa kwenda juu. Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu. 2Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu. 3Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu? 4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu. 5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari! 6Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani. 7Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.