Psalms 127
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure. 2Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake. 3Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake. 4Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. 5Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.