Psalms 128
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Wimbo wa kwenda juu. Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake. 2Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. 3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. 4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana. 5Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, 6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.