Psalms 54
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. 2Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu. 3Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu. 4Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza. 5Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize. 6Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema. 7Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.