Psalms 57
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni. Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite. 2Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. 3Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. 4Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali. 5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. 6Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe. 7Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 8Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. 9Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 10Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, uaminifu wako unazifikia anga. 11Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, utukufu wako na uwe duniani pote.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.