Psalms 82
Choose a chapter
123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150
1Zaburi ya Asafu. Mungu anaongoza kusanyiko kuu, anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”: 2“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki na kuonyesha upendeleo kwa waovu? 3Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. 4Mwokoeni mnyonge na mhitaji, wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu. 5“Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. 6“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”; ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’ 7Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida; mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.” 8Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ (Open Kiswahili Contemporary Version) © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under CC BY-SA 4.0.